NEWS

Saturday 24 September 2022

Shelutete atemwa TANAPA


Pascal Philemon Shelutete

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetangaza kusitisha utumishi wa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Pascal Philemon Shelutete na Afisa Uhifadhi Mwandamizi, Justin Jackson Lema, kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.

Kwa mujibu wa tangazo kwa umma na wadau wa uhifadhi na utalii, lililotolewa na TANAPA na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii leo, utumishi wa Shelutete na Lema katika shirika hilo umekoma kuanzia Septemba 15, 2022.

“Shirika [yaani TANAPA] halitahusika na jambo lolote watakalojihusisha nalo kwa niaba ya shirika,” imeeleza sehemu ya tangazo hilo lililoambatanishwa na picha za Shelutete na Lema.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages