NEWS

Friday, 30 August 2024

Rwanda: Rais Kagame awafuta kazi wanajeshi zaidi ya 200



Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
------------------------------------------

Rais wa Rwanda Paul Kagame amewafuta kazi wanajeshi 214, wakiwemo maafisa kadhaa wakuu wa kijeshi.

Taarifa fupi ya Wizara ya Ulinzi ya Rwanda, iliyowekwa kwenye ukurasa wake rasmi wa X asubuhi ya leo, imesema maafisa waliofutwa kazi ni pamoja na Meja Jenerali Martin Nzaramba na Kanali Dkt Etienne Uwimana.

"Pia ameidhinisha kufutwa na kubatilishwa kwa maafisa 195 wa vyeo vingine vya Jeshi la Ulinzi la Rwanda," imesema taarifa hiyo.

Hakuna sababu iliyotolewa kwa hatua hiyo, lakini ilitangazwa saa chache baada ya Kagame kukutana na maafisa wakuu wa kijeshi, akiwemo Mkuu wa Majeshi Jenerali Mubarakh Muganga.

Tovuti inayounga mkono serikali ya New Times, imeripoti kwamba Rais Kagame na maafisa wa kijeshi wamejadili vipaumbele vya amani na usalama vya Rwanda.
Chanzo: BBC
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages