Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko (wa pili kulia mbele) akikagua mradi wa maendeleo wilayani Kakonko, Kigoma leo.
--------------------------------------
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko amesema serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuupatia mkoa wa Kigoma miradi ya maendeleo na fursa mbalimbali za kuufungua kiuchumi.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Kasanda wilayani Kakonko, Kigoma leo Septemba 18, 2024, Dkt Biteko amesema serikali imetekeleza miradi mingi ya maendeleo, ikiwemo hospitali na barabara - ikilinganishwa na kipindi kilichopita ambapo wananchi walikuwa wakitaabika kupata huduma mbalimbali za kijamii.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Iranian hackers allegedly shared Trump campaign data with Biden associates, FBI reports
>>Mwenyekiti Halmashauri ya Serengeti atembelea ofisi za Gazeti la Sauti ya Mara
>>Nyambari apokea kundi la wafanyabiashara maarufu kutoka India, wafanya ziara Zanzibar
>>CSR Mgodi wa Barrick Bulyanhulu yawagusa watu wenye ulemavu Msalala
No comments:
Post a Comment