Mwenyekiti wa MRPC, Jacob Mugini (kulia) akimkabidhi Meneja Mkuu wa WAMACU Ltd, Samwel Gisiboye cheti cha shukrani katika ofisi za ushirika huo mjini Tarime jana. Kushoto ni Meneja wa Shughuli na Biashara, Olais Piniel.
----------------------------------------
Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC) imekitunuku Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Mara (WAMACU Ltd) cheti cha shukrani kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za kuutangaza mkoa huo kama sehemu bora kwa uwekezaji.
Mwenyekiti wa MRPC, Jacob Mugini alikabidhi cheti hicho kwa Meneja Mkuu wa WAMACU Ltd, Samwel Gisiboye katika ofisi za ushirika huo mjini Tarime, jana Septemba 10, 2024.
Ushirika wa WAMACU unatajwa kuwa na mchango mkubwa katika kuleta mageuzi ya maendeleo kwa wakulima wa kahawa na tumbaku, miongoni mwa mazao mengine mkoani Mara.
No comments:
Post a Comment