NEWS

Monday, 4 November 2024

Nyambari Nyangwine Foundation yagawa msaada wa vitabu kwenye sekondari za Halmashauri ya Tarime Mji, wanafunzi waahidi matokeo mazuri



Msemaji wa Nyambari Nyangwine Foundation, Jacob Mugini akizungumza na wanafunzi alipokwenda kukabidhi msaada wa vitabu katika Shule ya Sekondari Iganana iliyopo Halmashauri ya Mji wa Tarime leo Novemba 4, 2024.
------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

TAASISI ya Nyambari Nyangwine (NNF) kwa mara nyingine, imeanza kugawa msaada wa vitabu vya kiada na ziada kwenye shule za sekondari mbalimbali zilizopo Halmashauri ya Mji wa Tarime, mkoani Mara.

Usambazaji wa msaada huo umeanza rasmi leo Novemba 4, 2024, ambapo shule sita - za Nyamisangura, Iganana, Angel House, Bomani, Nkende na Rebu zimekabidhiwa vitabu vyenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni 12.


Makabidhiano ya vitabu katika Shule ya Sekondari Nyamisangura,
--------------------------------------------

Msemaji wa Nyambari Nyangwine Foundation, Jacob Mugini amesema hatua hiyo ni ya kuunga mkono juhudi za serikali kwenye uwekezaji na uboreshaji wa maendeleo ya elimu.


Makabidhiano ya vitabu katika Shule ya Sekondari Bomani.
--------------------------------------------

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo wa vitabu, Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyamisangura, Mwalimu Zacharia Kabengo ameishukuru taasisi hiyo akisema vitawapunguzia changamoto iliyokuwepo.

"Tunaishukuru sana Nyambari Nyangwine Foundation, nimefarijika sana kwa msaada huu wa vitabu, hususan vya masomo ya sanaa. Tutavitunza na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa," amesema Mwalimu Kabengo.


Makabidhiano ya vitabu katika Shule ya Sekondari Iganana.
------------------------------------------


Makabidhiano ya vitabu katika Shule ya Sekondari Nkende.
---------------------------------------------

Naye mwanafunzi wa Sekondari ya Nyamisangura, Rahma Maswi akizungumza kwa niabata wanafunzi wa shule hiyo ameishukuru taasisi hiyo na kuahidi kusoma kwa bidii

"Tunaahidi kufanya vizuri, kupitia hivi vitabu watapatikana watu wakubwa - madaktari, walimu, wanasheria na wataalamu wengine," amesema Rahma.


Makabidhiano ya vitabu katika Shuleya Sekondari Angel House.
-------------------------------------------

Katika shughuli ya usambazaji wa vitabu, Msemaji wa NNF ameambatana na baadhi ya madiwani wa viti maalum kutoka chama tawala - CCM, ambao wameishukuru Taasisi ya Nyambari Nyangwine kwa msaada huo muhimu wa kielimu.


Msemaji wa Nyambari Nyangwine Foundation, Jacob Mugini (mwenye tai) akikabidhi msaada wa vitabu kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Rebu mjini Tarime.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages