NEWS

Sunday, 3 November 2024

Rais Samia ataja mambo yatakayowezesha Tanzania kuwa ghala la chakula barani Afrika



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye mjadala (round tables discussion) wa kimataifa kuhusu kilimo barani Afrika, uliofanyika nchini Marekani jana.
-----------------------------------------

Na Mwandishi Wetu

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, akiwa kwenye mkutano wa kimataifa nchini Marekani, ametaja mambo makuu matatu ya kuinusuru Tanzania kukumbwa na janga la njaa siku za usoni.

Mambo hayo ni kuifanya Tanzania kuongeza uzalishaji chakula maradufu, kupunguza hasara itokanayo na upotevu wa chakula baada ya mavuno na kuigeuza nchi kuwa ghala la chakula katika maeneo ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Akishiriki katika mjadala wa kimataifa wa kilimo kuhusu Afrika uliotayarishwa na Shirika la World Food Prize Foundation jijini Des Moines, jimbo la Lowa, Marekani jana, Rais Samia alisema Tanzania inakusudia kudhibiti ubora wa chakula kinachozalishwa, kusimamia bei yake na kuhakikisha upatikanaji wake kwa walaji.

Kuhusu kupunguzwa kwa hasara itokanayo na upotevu wa chakula baada ya mavuno, alisema serikali yake itaweka mkazo zaidi kwenye ujenzi wa maghala ya hifadhi na miundombinu mingine muhimu.

Mjadala huo wa usalama wa chakula kwa bara la Afrika pia ulihudhuriwa na viongozi wa bara hilo na wadau wa sekta binafsi nchini Marekani wanaojishughulisha na kilimo.

Mkutano huo ulikuwa ni sehemu ya matukio ya Taaissi ya Norman E. Borlaug International Dialogue inayojishughulisha na masuala ya usalama wa chakula na kilimo.

Ni mkutano wa ngazi za juu unaowakutanisha viongozi wa dunia na wataalamu wa maendeleo, kilimo, sera za uchumi, menejimenti ya rasilimali na lishe.

Pia, ni mkutano unaofuatiwa na kutolewa kwa tuzo kubwa ya World Food Prize inayofanana na ile ya Nobel. Tuzo hiyo hutolewa kwa watu waliojipambanua kupambana na janga la njaa duniani.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages