NEWS

Sunday, 29 December 2024

Korea Kusini:Zaidi ya watu 170 wafariki dunia katika ajali ya ndege

Sehemu ya mabaki ya ndege hiyo iliyopata ajali Korea Kusini
----------------------------------------

Ndege iliyokuwa imebeba abiria 181 imeanguka katika uwanja wa ndege kusini magharibi mwa Korea Kusini.

Ajali hiyo ilitokea muda mfupi baada ya 09:00 saa za eneo - 00:00 GMT - wakati ilipokuwa ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muan.

Picha zinaonekana kuonyesha ndege hiyo ikiteleza kutoka kwenye njia ya kurukia na kuangukia ukuta, kabla ya baadhi ya sehemu zake kuwaka moto.

Shirika la Kitaifa la Zimamoto limethibitisha sasa kwamba watu 167 walifariki katika ajali hiyo ya ndege.

Hapo awali, tulisikia pia kwamba wafanyikazi wawili wa ndege walipatikana wakiwa hai na kusafirishwa hadi hospitalini.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Muan wa ukubwa wa kati ulifunguliwa mwaka wa 2007, na una njia za kwenda nchi kadhaa za Asia.
Chanzo:BBC
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages