NEWS

Saturday, 21 December 2024

Mara Press haitafanya kazi na online TV, blogs ambazo hazijasajiliwa TCRA – Mugini



Mwenyekiti wa MRPC, Jacob Mugini akizungumza katika semina kwa waandishi wa habari wa mkoani Mara iliyoandaliwa na TCRA Kanda ya Ziwa na kufanyika mjini Musoma jana.
--------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Musoma

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC) imesisitiza msimamo wake wa kutafanya kazi na vyombo vya habari vya mtandaoni zikiwemo online tv na blogs zinazojiendesha kiholela bila kuwa na usajili kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

“Tukifanya kazi na vyombo ambavyo havina usajili tutakuwa sehemu ya uchafu, jambo ambalo halina tija kwa maendeleo ya sekta ya habari,” Mwenyekiti wa MRPC, Jacob Mugini amesema.

Mugini alikuwa akizungumza katika semina ya kuwajengea waandishi wa habari wa mkoani Mara uelewa kuhusu umuhimu wa leseni za maudhui ya vyombo vya mtandaoni, iliyoandaliwa na TCRA Kanda ya Ziwa na kufanyika mjini Musoma jana Desemba 20, 2024.

Aidha, Mwenyekiti huyo aliishukuru TCRA kwa kuandaa na kuendesha semina hiyo muhimu akisema itakuwa chachu ya maendeleo ya sekta ya habari mkoani Mara.


Meneja wa TCRA Kanda ya ZIwa, Mhandisi Imelda Salum akizungumza.
------------------------------------

Awali, akiwasilisha mada katika semina hiyo, Mhandisi Aude Kileo kutoka TCRA alisema hadi sasa idadi ya vyombo vya habari vya mtandaoni vilivyopo mkoani Mara vinavyotambuliwa na mamlaka hiyo ni saba pekee.

Mhandisi Kileo alivitaja vyombo hivyo vyenye leseni za maudhui mkoani Mara kuwa ni pamoja na Mara Online News, DIMA Online, Lake Zone Watch, George Marato TV, Kitaji Ndoto Yetu Initiative na Cleo Online TV.

Picha ya pamoja baada ya semina hiyo. Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages