NEWS

Sunday, 21 July 2024

Biden ajiondoa kwenye kinyang’anyiro cha urais Marekani



Joe Biden
-----------------

Hatimaye Rais wa Marekani, Joe Biden ametangaza kusitisha kampeni za kuwania muhula wa pili, akisema amechukua uamuzi huo “kwa maslahi ya chama chake na nchi.”

Uamuzi wa Biden kujitoa kwenye mbio za urais huku ikiwa imesalia miezi minne kabla ya Wamarekani kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu.

Kwa wiki kadhaa sasa, Biden amekuwa akishinikizwa na wanachama wenzake wa chama cha Democrats ajitoe kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kufanya vibaya kwenye mjadala na mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump mwishoni mwa Juni 2024.

Katika barua aliyoituma kupitia mitandao yake ya kijamii leo Julai 21, 2024, Rais Biden amesema imekuwa ni fahari ya maisha yake kuhudumu kama rais.

“Na ingawa imekuwa nia yangu ya kutaka kuchaguliwa tena, naamini ni kwa manufaa ya chama changu na nchi kwa mimi kujiondoa na kuzingatia tu kutimiza wajibu wa Rais kwa kipindi kilichosalia cha muhula wangu,” amesema Biden.
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages