
Mwenyekiti wa NNGCL, Nyambari Nyangwine (wa nne kutoka kushoto), akiwa katika ziara ya kibiashara nchini Uganda, Novemba mwaka huu.
Nyambari Nyangwine Group of Companies Ltd (NNGCL) sasa imeeneza mtandao wake katika nchi za Afrika Mashariki na Kati na kujitwalia umaarufu katika nchi hizo, Mara Online News inaweza kuripoti.
NNGCL, yenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam, Tanzania, ni kielelezo thabiti cha azma ya mwanzilishi wake, Nyambari Nyangwine, ya kuwa kitovu cha ubora, ubunifu na uboreshaji wa maisha ya jamii.
Kwa sasa NNGCL inaendesha shughuli za kibiashara ikiwa na ofisi ndogo katika miji mikuu ya Nairobi (Kenya), Kampala (Uganda), Kinshasa (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo) na Lusaka (Zambia).
NNCGL inajumuisha kampuni tanzu kadhaa ambazo ni pamoja Nyambari Nyangwine Agri-Business inayojishughulisha na kuimarisha tija na kilimo endelevu.
Kampuni nyingine ni Nyambari Nyangwine Bookshop ambayo imejikita kwenye kuinua elimu kupitia uuzaji wa vitabu muhimu vinavyohitaji shuleni.

Mwenyekiti wa NNGCL, Nyambari Nyangwine, akishirii kwenye uzinduzi wa taasisi yake ya Nyambari Nyangwine Foundation jijini Dar es Salaam, Septemba mwaka huu.
Pia, kuna Kampuni ya Nyambari Nyangwine Sky Media ambayo inajishughulisha na vielelezo na majukwaa ya mtandaoni kwa ajili ya kuwasaidia watu wanaotafuta fursa za mafunzo.
Kampuni nyingine ya Nyambari Nyangwine Publishers imeanzishwa rasmi ili kukidhi mahitaji ya wateja kwa huduma za kisasa za teknolojia ya uchapishaji.
Kwa masuala ya kuiwezesha jamii kwa huduma za fedha na mafunzo ya elimu, ni jukumu linalobebwa na Kampuni ya Nyambari Nyangwine Microfinance, wakati kampuni ya Nyambari Nyangwine (T) Ltd inashughulikia matumizi endelevu ya raslimali.
Kampuni nyingine inayochipuka kwa kasi ni ile ya Nyambari Nyangwine Civil & Building Construction iliyoweka kipaumbele kwenye ujenzi bora na ukabidhi wa miradi kwa muda uliopangwa.
Chini ya kampuni mama ya NNGCL, upo msululu wa kampuni nyingine kama vile Nyambari Nyangwine Partnership Academy ambayo inashughulika na utoaji elimu bora na nafasi za kujiendeleza.

Mwenyekiti wa NNGCL, Nyambari Nyangwine (aliyevaa kofia), akiwa kwenye ziara ya biashara nchini India, Julai mwaka huu.
Imo pia Nyambari Nyangwine One Family Hospital inayoshughulikia afya bora kwa jamii na Nyambari Nyangwine Foundation inayosaidia maendeleo ya jamii, uingizaji wa teknolojia katika elimu na masuala mengine ya maisha.
Nayo Kampuni ya Nyambari Nyangwine General Supply inabeba jukumu la kufikisha bidhaa mbalimbali kwa wateja wakati Kampuni ya Nyambari Nyangwine Security Equipment inejikita katika kuweka vifaa vya usalama.
Kampuni nyingine ya Nyambari Nyangwine Consultants inatoa huduma za kitaalamu za ushauri katika maendeleo ya biashara, elimu, fedha, utafiti na utungaji wa sera.
Mwenyekiti wa NNGCL, Nyambari Nyangwine, ambaye pia ni mwandishi, mchapishaji na msambazaji maarufu wa vitabu nchini Tanzania, anasema "Shughuli kubwa ni biashara ambayo inaendeshwa kwa mkakati wa uchambuzi wa soko, utambuzi wa watoa huduma na ujenzi wa uhusiano na wateja."
No comments:
Post a Comment