
Angelina Lubala Mabula
Na Mwandishi Wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Angelina Lubala Mabula kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Mabula anachukua nafasi ya Beno Morris Malisa ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Aidha, Rais Samia amemteua Dunford George Mpelumbe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kuchukua nafasi ya Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mwaimu aliyemaliza muda wake.
Naye Omar Ali Omar ameteuliwa na Rais Samia kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kuchukua nafasi ya Mohamed Khamis Hamad aliyemaliza muda wake.
Uapisho wa viongozi wateule hao utafanyika tarehe itakayopangwa baadaye, kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Shaaban Kissu.
No comments:
Post a Comment