NEWS

Tuesday 23 March 2021

Ondoeni mashaka nitaongoza Tanzania bila kutetereka – Rais Samia

Rais wa Jamhuri ya Muungno wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye shughuli ya kitaifa ya kuuaga mwili wa mtangulizi wake, Hayati Dkt John Pombe Magufuli jijini Dodoma.


RAIS wa Jamhuri ya Muungno wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameutaka umma kumwamini kuwa ni mwanamke mwenye uwezo wa kuiongoza nchi bila kutetereka.

 

“Kwa wale ambao wana mashaka, ‘mwanamke huyu ataweza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?’ Nataka niwaambie aliyesimama hapa ni rais… nataka nirudie, aliyesimama hapa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye maumbile yake ni mwanamke,” amesema Rais Samia.  

 

Rais Samia ameyasema hayo wakati alipowaongoza viongozi kutoka mataifa mbalimbali na Watanzania kwa ujumla katika shughuli ya kitaifa ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt John Pombe Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021.

         

Shughuli hiyo imefanyika Machi 22, 2021 kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, ambapo Rais Samia amesema yuko imara na ana uwezo mkubwa wa kuiongoza Taifa bila kuyumba. 

 

Amefafanua kuwa licha ya kuwa mwanamke, yuko imara kutokana na uwezo aliojengewa na mtangulizi wake, Dkt Magufuli ambaye hakuwa mtu wa kuyumbishwa bali mwenye msimamo thabiti kwa kile alichoamini kina maslahi kwa Watanzania. 

 

Rais huyo amesema yeye na viongozi wenzake wako tayari kuiendeleza miradi yote iliyoanzishwa na serikali chini ya uongozi wa Dkt Magufuli.

 

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages