NEWS

Tuesday 6 February 2024

Maadhimisho Miaka 47 ya CCM: Wananchi Musoma Vijijini waishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwaboreshea huduma za kijamiiMgeni rasmi akipokewa kwenye maadhimisho ya kumbukizi ya Miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika Musoma Vijijini jana.
-------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Musoma
-----------------------------------------


WANANCHI Musoma Vijijini wameadhimisha kumbukizi ya Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kutumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuwaboreshea maisha yao kupitia huduma mbalimbali za kijamii.

Wakizungumza wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho hayo zilizofanyika katika kijiji cha Seka kilichopo kata ya Nyamrandirira, Wilaya ya CCM ya Musoma Vijijini jana, wananchi hao walimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuidhinisha fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo yao ya kijamii.

Aidha, walimpongeza Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kwa jitihada kubwa anazofanya kuwaletea maendeleo ya kisekta.


Prof Sospeter Muhongo
---------------------------------
“Tunamshukuru Mbunge wetu Profesa Muhongo, anajitahidi sana kuhakikisha changamoto zinazowakabili wakazi wa jimbo hili la Musoma Vijijini zinaisha,” alisema mmoja wa wananchi hao.

Walisema jimbo hilo linaendelea kupiga hatua kubwa katika uboreshaji huduma za kijamii, hasa elimu, afya, maji na barabara.

Kwa upande wake, mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Ibrahim Mjanaheri Ibrahim aliwataka wananchi hao kuendelea kuwaamini viongozi wao, akisisitiza kuwa chama hicho tawala kimejiandaa kuhakikisha changamoto zote zinazowakabili zinapatiwa ufumbuzi.


Mjanaheri akihutubia maadhimisho hayo
-------------------------------------

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages