NEWS

Monday, 16 June 2025

Wadau wa sekta ya madini kujadili ‘Local Content’ kwa siku tatu kuanzia leo jijini Mwanza



Lori likiwa kazini mgodini

Na Mwandishi Wetu

Wadau mbalimbali wa sekta ya madini nchini watakutana jijini Mwanza kwa siku tatu kuhudhuria Jukwaa la Nne la Utekelezeaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya Madini (LCCF2025) kuanzia leo Juni 16 hadi 18, 2025.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, alisema jukwaa hilo litakalofanyika katika hoteli ya Malaika Beach Resort.

Kaulimbiu ya jukwaa hilo kwa mwaka huu ni “Increased Local Participation in the Mining Industry: A Catalyst for Tanzania’s Economic Growth” ambayo inahamasisha ushiriki wa Watanzania katika sekta ya madini ili kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.

Mhandisi Lwamo alisema jukwaa hilo litawakutanisha washiriki kutoka serikalini, sekta binafsi, asasi za kiraia na washirika wa maendeleo kutathmini maendeleo, kubadilishana uzoefu na mikakati ya kukuza maudhui ya ndani katika sekta ya madini Tanzania.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika jukwaa hilo ambalo linafanyika katika mikoa ya kanda ya ziwa ambayo inafanya vizuri katika uzalishaji wa dhahabu nchini. Baadhi ya mikoa hiyo ni Mara, Shinyanga na Geita.

Akitilia mkazo umuhimu wa ushiriki wa ndani katika kumiliki na kukuza sekta ya madini ili isaidie katika uchumi wa taifa, Mhandisi Lwamo alizitaka kampuni, watoa huduma, wawekezaji watunga sera na wananchi kushiriki kikamilifu katika majadiliano hayo.

“Jukwaa linatoa nafasi kwa mjadala madhubuti na wenye ushiriki wa kila mdau ili kuhakikisha kwamba Tanzania inanufaika na tasnia ya madini,” Mhandisi Lwamo alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages