MKUU wa Wilaya ya Tarime (DC) Col. Michael Mntenjele amezindua rasmi zoezi la kutoa chanjo dhidi ya UVIKO-19 (Corona) na kuwataka wananchi walio katika makundi yanayolengwa kujitokeza kupata chanjo hiyo.
DC Mntenjele pamoja na Katibu Tawala (DAS) wa wilaya hiyo
John Marwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya wamechanjwa
wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo ambalo limefanyika mapema leo Agositi 6,2021
katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime
![]() |
DC Tarime akipata chanjo dhidi ya UVIKO-19 |
Aidha mkuu huyo wa wilaya amekemea watu wanatoa tarifa za upotoshaji kuhusiana na chanjo hiyo na kuwataka wananchi kuwapuuza.
Amesema pia suala kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virus vya Corona
lazima yaendelee kuzingatiwa hata kwa wale ambao watachanjwa.
“Pamoja na kuwa tutakuwa tumepata chanjo hatua
zingine za kujikinga na kuwakinga wengine ziendelee kuchukuliwa”, amesisitiza
DC Mntenjele.
![]() |
DC Mntenjele akiongea na wananchi waliojitokeza kupata chanjo leo Ijumaa |
Aidha katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi jana alizindua zoezi la kutoa chanjo dhidi ya UVIKO-19 kimkoa mjini Musoma jana.
DAS Marwa akipata chanjo ya UVIKO-19 |
No comments:
Post a Comment