NEWS

Tuesday, 14 July 2026

Rais Samia amteua Asha Dachi kuwa Mkurugenzi Mkuu TBC



Asha Dachi Mbaruk

Na Mwandishi Wetu
---------------------------

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Asha Dachi Mbaruk kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu leo Jumanne, imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo, Mbaruk alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).

Mbaruk anachukua nafasi iliyoachwa na Dkt. Ayub Rioba Chacha ambaye amemaliza muda wake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages