Na Mwandishi Wetu
Baraza la Uongozi la Akademia ya Sayansi Afrika (AAS) limezinduliwa rasmi kuendesha shughuli zake.
Sherehe ya uzinduzi wa Baraza hilo ilifanyika leo Jumatatu jijini Nairobi, Kenya na kuhudhuriwa na wanazuoni mashuhuri Afrika, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Makamu wa Rais, Kanda ya nchi za Mashariki ya Afrika.
Prof Muhongo, msomi maarufu nchini Tanzania na bingwa wa masuala ya jiolojia, ni miongoni mwa wanazuoni mashuhuri wa Afrika waliohudhuria uzinduzi wa Baraza hilo la AAS.
Viongozi wengine waliohudhuria sherehe hiyo ni Rais wa AAS, Prof Friday Okonofua wa Nigeria, Katibu Mkuu, Prof Francine Ntoumi (Congo Brazzaville), Mhazini, Prof Stephen Agong (Kenya), Makamu wa Rais, Kanda ya Kusini mwa Afrika, Prof Kenneth Ozoemena, Makamu wa Rais, Kanda ya Afrika ya Kati, Prof Felix Toteu, Makamu wa Rais, Kanda ya Afrika Magharibi, Prof Balla Diop Ngom, na Prof Rajaa Cherkaoui wa Kanda ya Afrika Kaskazini.

Prof Muhongo anasimamia nchi 14 za Burundi, Comoro, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mauritius, Rwanda, Shelisheli, Somalia, Afrika Kusini, Tanzania na Uganda.
No comments:
Post a Comment