SACP Henry Mwaibambe |
Na mwandishi wetu, Tarime
Mkuu wa shule ya sekondari ya Kenyamanyori Zakaria
Kabengo jana usiku alishambuliwa vibaya na majambazi waliovamia nyumbani kwake
Rebu Majengo mapya katika Mji wa Tarime Mkoani Mara.
Hata hivyo mwalimu huyo alikosa matibabu kwa zaidi
ya saa moja katika hospitali ya Wilaya ya Tarime kutokana na ukosefu wa umeme na mafuta ya jenereta.
“ Majambazi hawa waalinza kunishambulia leo majira ya saa tatu usiku baada ya kuona mmoja wao anamlika tochi, nilipohoji wewe ni nani walianza kunikatakata mapanga na mwingine
akajitokeza na kutishia kunipiga risasi
endapo ningeendelea kupiga kelele. Waliendelea
kunishambulia huku wakitaka niwape pesa “, alisema Kabengo muda mfupi baada ya shambulio hilo wakati
akisubiri matibu katika hospitali ya wilaya hiyo.
Majambazi hao walitokemea baada ya mke wa Kabengo
kuwarushisa shilingi laki moja kupitia dirishani.
“ Nilimwambia mke wangu awape laki moja tuliyokuwa nayo
ndani na majambazi walitaka awarushie kupitia dirishani”, alisema Mwalimu
Kabengo huku akionesha kuhuzunishwa na tukio hilo la kinyama .
Polisi walifika nyumbani kwa mwalimu Kabengo mara
baada ya tukio.
Juhudi za Mara Online News kumtafuta Kamanda wa Polisi
Kanda Maalumu ya Tarime Rorya(RPC) Henry Mwaibambe kuzungumzia tukio hilo bado
zinaendelea.
No comments:
Post a Comment