NEWS

Monday 5 August 2019

DEREVA WA RC MARA NA MTOTO WAKE CHINI YA ULINZI MKALI WA POLISI - RPC





Na Mwandishi Wetu ,Musoma

Dereva wa gari la Mkuu wa Mkoa wa Mara  na mtoto wake wako chini ya mikono ya jeshi la polisi  baada kijana wa dereva huyo kuchukua gari la serikali analotumia Mkuu wa Mkoa  na kisha kupata ajali jana Jumapili.
Hata hivyo dereva huyo wa Mkuu wa Mkoa alipoteza fahamu baada ya tukio hilo kutokea  na kulazwa katika hospitali ya Mkoa wa Mara mjini Musoma.
Kijana wa dereva huyo  pia  alilazwa katika hospitali hiyo ya Mkoa wa Mara baada ya kupata majeraha katika ajali hiyo .
“ Hali zao zinaendelea vizuri na wako hospitalini chini ya ulinzi mkali wa polisi” Kamanda wa Polisi Mkoa(RPC) wa Mara Juma Ndaki ameimbia Mara Online News leo mchana.
Kamanda Ndaki hakupenda kutaja majina yao kwa sasa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages