Na Clonel Mwegendao
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ametoa
baraka kwa Wilaya ya Tarime kufungua masoko mawili ya kuuza madini ya dhahabu katika
eneo la Nyamongo na Tarime Mjini .
Naibu Waziri
Nyongo ametaka masoko hayo kuanza
kufanya kazi kesho Julai 6.
“ Naomba
kusema rasmi kuanzia tarehe 6 masoko ya Nyamongo na Tarime yafunguliwe rasmi ,
hakuna mjadala wa hilo”, Nyongo alisisitiza
wakati akiongea na wachimbaji wadogo na wadau wengine wa sekta ya madini katika chuo cha Ualimu Tarime jana jumapili.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime(DC) Charles Kabeho amesema kufunguliwa kwa masoko hayo kutasogeza huduma
karibu kwa wachimbaji wa dhahabu wa Nyamongo na Mji
wa Tarime .
Hatua hiyo pia inatarajiwa kupunguza utoroshwaji wa
dhahabu kwenda nchi jirani kwa njia ya magendo.
“ Natambua soko la madini ya
dhahabu lipo Musoma
lakini na nia yetu ni kusogeza
huduma kwa wachimbaji . Kuna baadhi ya
watu wakitoka tu kwenye mashimo
wanahitaji fedha ya dharula na kusafiri kwenda Musoma wanaona ni mbali“,
alisema Kabeho .
TAZAMA VIDEO
No comments:
Post a Comment