Hatimaye hospitali ya Wilaya ya Serengeti imeanza kutoa
huduma kwa wananchi baada ya ujenzi wa
baadhi ya majengo muhimu kukamilika.
Baadhi ya huduma ambazo zimeanza kutolewa katika hospitali hiyo ni chanjo na kiliniki ya mama na mtoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Serengeti Mhandisi Juma Hamsini anasema hilo
limewezekana baada ya serikali ya awamu
ya tano kuwapatia shilingi milioni 800.
Fedha hizo zimetumika
kukamilisha na kuanzisha ujenzi wa baadhi
ya majengo katika Hospitali hiyo
ambyo inaelezwa itakuwa ya kisasa baada
ya ujenzi wake kukamilika .
“ Hadi
sasa tumepokea shilingi milioni 800 na zaidi ya shilingi milioni 680
zimetumika kuboresha majengo
yanayoonekana na kazi inaendelea “, Hamsini aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibuni .
“
Tayari hospitali hii imeanza kutoa huduma kama
vile chanjo, kliniki ya mama na mtoto
na ndani ya wiki moja kuanzia sasa wajazawazito wataanza
kujifungulia hapa”, aliongeza Hamsini.
Wananchi wa mji wa Mugumu na vijiji jirani wanaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutoa fedha ambayo imesadia kuharakisha ujenzi wa
hospitali hiyo.
“ Napenda kumshukuru Mhe Rais
John Magufuli kwa mchango wake ambao ametoa kwa ajili ya
ujenzi wa hospitali yetu ya Wilaya .Tunaomba mheshimiwa Rais
aendelee kutuongezea vitendea
kazi ili watoto na wajawazito wasife “, anasema Mama Maiko ambaye ni
mjasirimali katika soko la Mugumu .
DED Serengeti Mhandisi Juma Hamsini( wapli kulia) na Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi waHospitali ya Wilaya ya Serengeti Charles Chacha ( wakwanza kushoto) wakikagua kazi inavyoendelea hivi karibuni. |
Kutokana na kiu iliyokuwepo
kwa wananchi wa Serengeti kupata
Hospitali ya wilaya , baadhi ya wazee
walijitolea kusimamia ujenzi wa
hospitali hiyo bila kuchoka .
“ Hospitali yetu hii
itakapokamilika itakuwa ni fursa nzuri sana kwa wakazi wa
Serengeti lakini pia itakuwa fursa kwa watu wengine kutoka maeneo mbalimbali”,
Jambo la kufurahisha ni kwamba
tayari ofisi za Mganga Mkuu wa Wilaya zimeanza rasmi kufanya kazi katika jengo
la hospitali hiyo mpya ya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.
Ujenzi wa hosiptali hiyo ulianza katika serikali ya awamu ya nne
ambapo kwa kuanzia serikali ilitoa shilingi bilioni 1.6 kati ya mwaka 2009 na 2012 kwa ajili ya
maandalizi ya awali.
Hamsini anasema fedha hizo
zilitumika pamoja na mambo mengine kusafisha eneo la ujenzi kulipa fidia , kuweka mhandisi mshauri na kuanzisha ujenzi wa majengo ya OPD( jengo kwa ajili ya wagongwa wa nje ).
Mwaka 2011 benki ya Afrika(AFD)
ilifadhili ujenzi wa chumba cha upasuaji ( theater)na nyumba za watumishi na baada ya hapo ujenzi wa hospitali hiyo ulisimama
.
SAFARI IKAANZA TENA 2016
Ujenzi wa hospitali hiyo
ulisimama mwaka 2012 hadi mwaka 2016
baada ya viongozi waliokuwa wameteuliwa na Rais John Magufuli kuanzisha kampeni
ya jenga hospiliti kwa shilingi 1,000. Kampeni hiyo ilihusisha wananchi wa Serengeti
na kisha kuungwa mkono na wadau wengine .
“ Tulianza na shilingi milioni
2.6 baadae wadau wakaanza kuonekana,
watu wakachangia sementi, mchanga SENAPA
wakatoa milioni 50 , wenzetu wa WMA wakatoa milioni 100 na tukafanya kazi
ikaonekana”, anasema Mhandisi Hamsini.
Baada ya kuonesha juhudi hizo, Mhandisi Hamasini anasema Rais Magufuli aliwapatia shilingi milioni 400 kusaidia ujenzi wa hospiatali hiyo.
“ Milioni 400 ndo imependezesha
hayo majengo yanaonekena yana rangi na
umeme unawake lakini bado tulibaki na vifaa vingi”, anasema Mhandisi Hamsini.
Baada ya hapo Halmashauri hiyo
pia ilipokea shilingi milioni 400 zingine ambazo zinaendelea kukamilisha na
kuanzisha majengo mapya katika hospitali hiyo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Serengeti kwa vipindi vitatu tofouti
John Ng’oina ambaye hivi sasa ni diwani wa kata ya Mbalibari anasema
walianzisha ujenzi wa hospitali hiyo
kwa kuwa Wilaya hiyo ya Serengeti haijawahi kuwa na hospitali ya Wilaya ya Serikali jambo
lilikuwa ni tatizo kubwa kwa wananchi.
Ng’oina anasema jitahada za Mkuu wa Wilaya ya
Serengeti Nurdin Babu na wasaidizi wake
pamoja na shilingi milioni 800 ambazo zimetolewa na serikali ya awamu ya tano
zimeifikisha hosptalii hiyo mahali pazuri.
Jambo la kufurahisha ni
kwamba Halmashauri ya Serengti inagetemea
pia kupokea shilingi milioni 500 katika mwaka huu wa fedha kwa ajili ya
kuendeleza ujenzi wa hospitali hiyo.
“ Mwisho wa siku hospitali hii itakuwa ya
kisasa na itakuwa ikitoa huduma bora kwa wananchi wa Serengeti”, anasema
Mhandisi Hamsini.
No comments:
Post a Comment