Na Mwandishi Wetu
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Pindi Chana amesema mahusiano ya Kenya na Tanzania yameendelea kuimarika kutokana uongozi bora wa Rais John Magufuli na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta .
Dkt Chana alisema hayo juzi alipokuwa katika kilele cha maadhimisho ya nane ya siku ya Mara ambayo mwaka huu yalifanyika katika viwanja vya Sokoine Mjini Mugumu, Wilayani Serengeti.
Mataifa ya Tanzania na Kenya huadhimisha siku ya Mara Septemba 15 kila mwaka kwa lengo la kuweka mikakati ya kuhifadhi bonde la mto Mara .
“ Napenda kumpongeza Mhe Rais Magufuli na na Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta kwa kutuongoza vizuri na sasa tunasema,Tazania na Kenya sio majirani bali ni ndugu “, Balozi Chana alisema katika mahojiano na Mara Online News .
“ Maadhimisho haya ya Mara Day yanathibithisha kuwa sisi watanzania na wakenya tupo pamoja kujadili namna bora ya kutunza mazingira ya bonde la mto Mara “, alisema balozi huyo wa Tanzania nchini Kenya.
Dr Chana ambaye pia ni mwakilishi wa kudumu wa Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa ( United Nations Environment Programme) alisisitiza umuhimu wa kutunza mazingira kwa maendeleo endelevu.
No comments:
Post a Comment