Kamisheni
ya bonde la ziwa Victoria(LVBC) imezindua wimbo wa Mara ambao
unahamsisha utunzaji wa mazingira ya bonde la
Mara kwa upande wa Kenya na Tanzania .
Katibu
Mtendaji wa LVBC Dkt Ali –Saidi Matano alizindua wimbo huo Jumapili iliyopita mara tu baada ya kilele cha maadhimisho ya
nane ya siku ya Mara katika viwanja vya Sokine Mjini Mugumu Jana.
“ Wimbo huu umekuja kwa wakati mwafaka na tunaomba uimbwe kwenye redio,
runinga, madukani na hata kwenye mito wakati akina mama wanachota maji,
na wafugaji wakati wakiwa kwenye malisho ya mifugo yao nan a wanafunzi
mashuleni””, Dkt Matano alisema.
Dkt
Matano alishukuru shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na
Wanyamapori(WWF) kwa kuja na wazo la kutumia njia ya wimbo katika kuelimisha
jamii kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mto Mara .
.Wimbo
huo unamzungumzia mama akiwa kwenye shida analia akihataji msaada na mama
huyo ni mto Mara , alisema William Ojwang kutoka WWF Kenya .
“
Tunataka wimbo huu utumike kuendeleza kampeni ya kuhifadhi mto Mara na wimbo
huu uendelee kutukumbusha kuwa mama yetu(mto Mara) analia na anahitaji
msaada”,alisema Ojwang.
No comments:
Post a Comment