Na Mwandishi wetu,
Watuhumiwa 8 waliokamatwa wakiiba mawe ya dhahabu
yenye thamani ya zaidi ya milioni 200 ndani ya mgodi wa North Mara hivi karibuni
leo Oktoba 9, 2019 wamefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Tarime na
kusomewa mashitaka matano ikiwemo shitaka la uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.
Watuhumiwa hao ni Zabroni John Seth, James
Mahalareri Makune, Jonathan Chuwa Genji,Amos Raphael Wahere, Mseti Chacha
Isaka, Chacha Marwa Ryoba, Petro Kegora Mariba na Samson Mathoyo Leonard.
Wakati huo huo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo leo amezungumza
na waandishi wa habari mjini Tarime na kuonya wale wote
wanaoshiriki kufanya wizi wa mawe ya dhahabu katika mgodi North Mara kuacha mara moja.
No comments:
Post a Comment