Na mwandishi wetu,
Jumla watahiniwa 159 wa kidato cha IV 2019 wa shule ya sekondari Nkende iliyopo Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara wamemshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa kuwapatia elimu bure kwa miaka mine
mfululizo.
Wanafunzi hao
wameahidi kufaya vizuri katika mtihani wao ambao unatarajia kuanza mwezi ujao .
“ Kwa sababu sisi ndio wakwanza tunamuahidi Serikali na Rais wetu Kuwa tutafanya vizuri katika mithani yetu “,
amesema Faustina Ghati ambaye ni mmoj wa
watahiniwa wa kidato cha nne 2019 katika shule hiyo ya Nkende
"Baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakishindwa kufikia
ndoto zao kama vile kuwa madaktari kutokana na ukosefu wa ada,",amesema Rhobi Joseph Thomas ambaye pia ni
mtahiniwa katika shule hiyo ya Nkende.
Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo Gidion Chacha
amesema wanafunzi hao wameandaliwa vizuri kwa ajili ya kufanya mitihani yao.
Mkuu wa shule ya sekondari ya Nkende Samson Hagai
amesema mpango wa elimu bure umepunga
mzigo kwa wazazi .
“ Hata wanafunzi wenye uwezo darasani lakini
wanatoka kwenye familia ambazo zilikwa haziwezi kulipa ada sasa wanasoma bila
tatizo na idadi ya wanafunzi wanaojiunga
na elimu ya sekondari umeongezeka “, amesema Hagai.
Shule hiyo ya Nkende ina wanafunzi zaidi ya 800
ambao wananufaika na mpango wa elimu bure.
No comments:
Post a Comment