NEWS

Sunday 24 November 2019

DIPLOMASIA YA UCHUMI KATI YA KENYA NA TANZANIA KUIMARISHWA



Na Mwandishi wetu

Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dr Pindi Chana jana alitembelea  kituo cha pamoja cha forodha cha Holili - Taveta na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha diplomasia ya uchumi kati mataifa ya Tanzania na Kenya .



Balozi Pindi Chana aliwataka watumishi waliopo katika mpaka huo kuondoa vikwazo vyote visivyo vya kiforodha yaani non taarif –barriers.


“  Tujitahidi  kuwawezesha wafanyabisahara wa nchi zetu wanaotumia mpaka wa Holili – Taveta kuondokana kabisa na vikwazo visivyo vya kiforodha” , aliagiza balozi  Dr Chana.


Dr Pindi Chana  alisema mpaka wa Holili- Taveta ni muhimu katika kusafirisha bidhaa mbalimbali ikiwemo mazao aina ya vitunguu na mahindi  kutoka Tanzania  kwenda Mombasa nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages