NEWS

Friday 21 February 2020

Esther Matiko atembelea ofisi za Sauti ya Mara , akabidhi msaada wa kompyuta



Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko Jana Februari 21, 2020 alitembelea  ofisi za Mara Online na  kutekeleza ahadi yake kompyuta ambayo aliahidi mwezi uliopita katika hafla ya uzinduzi wa gazeti la Sauti ya Mara.

Matiko alipongeza Mara Online kwa kuanzisha gazeti la Sauti ya Mara ambalo hutoka kila siku ya Jumatatu na kusema gazeti hilo limeonesha mfano mzuri kwa kuripoti habari ambazo zimejikita zaidi katika maendeleo.

  Kwa kweli gazeti la Sauti ya  Mara ni gazeti ambalo linatoa habari za maendeleo bila kujali  ninani kafanya hayo maendeleo  “, Mbunge huyo alisema.
Aidha mbunge huyo alionesha kukunwa na timu ya vijana ambao ni wafanyakazi wa Mara Online na kuwaasa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwa na weledi ili waweze kufikia ndoto zao.


Mtendaji Mkuu wa Mara Online Jacob Mugini ambaye ni mwandishi wa habari alimshukuru  Mbunge Matiko kwa kuwatembelea na kuwapatia msaada wa kompyuta.

" Mheshimiwa tumefurahi sana kwa kututembelea na umetupa maneno mazuri ya kututia moyo", alisema Jacob


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages