NEWS

Tuesday 31 March 2020

Tanzania yathibitisha kifo cha kwanza cha Corona


WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Tanzania, Ummy Mwalimu amethibitisha kutokea kwa kifo cha kwanza cha mgonjwa wa Covid 19 (Corona) nchini humo kilichotokea leo Alfajiri Machi 31, 2020 katika kituo cha matibabu ya waathirika wa ugonjwa huo cha Mloganzila jijini Dar es Salaam.
 Mgonjwa huyo ambaye ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 49, pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine, kwa mujibu wa Waziri Mwalimu.
 Amesema hadi leo Alfajiri, rekodi inaonesha kuwa Tanzania ilikuwa na wagonjwa 19 wa Covid 19, mmoja aliyepona ugonjwa huo na kifo kimoja cha huyo aliyefariki dunia leo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages