Wakazi
wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara wameingiwa hofu kwamba huenda wakashindwa
kumudu kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona au COVID-19 baada ya
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) kutangaza
kusimamisha usambazaji wa huduma ya maji kwa muda usiojulikana.
Wananchi
hao wameeleza kustushwa na taarifa hiyo ya MUWASA hasa ikizingatiwa kuwa maji
ndiyo silaha kubwa ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo, ambapo wataalamu
wa afya na serikali wanahimiza watu kunawa mikona kwa sabuni na maji
yanayotiririka mara kwa mara.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na ofisi ya Uhusiano MUWASA leo Jumatano
Aprili 29, 2020, uzalishaji maji ya bomba umesimama kuanzia jana Jumanne Aprili
28, 2020 saa 12 jioni kutokana na hitilafu ya umeme katika kituo cha kuzalisha
maji Bukanga.
No comments:
Post a Comment