NEWS

Tuesday 28 April 2020

Watalaamu wachukua sampuli za maji mgodi ulioua mifugo


Watalaamu wa ubora wa maji kutoka Ofisi ya Dakio la Mara Mori leo wamechukua  sampuli za maji  kutoka kwenye mgodi  unaodaiwa kutiririsha maji yenye kemikali ya sumu ambayo iliua ng’ombe 34  na kondoo mmoja katika kijiji cha Kewanja jana April 27,2020 kwa ajili ya kufanyiwa uchungizi  .

“ Mpango wa Dakio ni  kutembelea na kukagua wachenjuaji wote wadogo na wa kati ili kuona mioundo mbinu ya ,maji wanayotumia kama ni rafiki wa mazingira”, Ofisa wa Dakio la Mara Mori  Mhandisi Mwita Mataro ameiambia Mara Online News mara baada ya kukamilisha zoezi hilo.
Mhandisi Mwita amesema mpango huwa utasaidia kuzuia madhara kama yalijitokeza jana pamoja na kulinda vyanzo vya maji 

1 comment:

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages