Ng’ombe 36 na kondoo mmoja wamekufa leo April 27 asubuhi katika kijiji cha
Kewanja kilichopo Nyamongo wilayani Tarime baada ya kunywa maji yanayohofiwa
kuwa na kemakali za sumu inayotokana na
maji yanayosafisha mawe ya dhahabu.
“ Ng’ombe waliokufa ni 36 na kondoo mmoja. Inahisiwa
wamekunywa maji yenye yenye kemikali ya simu yanayotiririka kutoka kwenye seneti za wachimbaji wadogo”,
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Kewanja Bunini John ameiambia Mara Online News dakika
chache zilizopita.
Mwenyekiti
huyo amesema Ng’ombe waliokufa ni wa familia mbili katika kitongoji cha Kemambo.
Watu wamezuiwa kuchota maji katika eneo la tukio .
" Habari na Mwandishi Wetu, Nyamongo)
" Habari na Mwandishi Wetu, Nyamongo)
asanteni kwa habari ila jitahidini kutoa breaking news pia habari na matukio motomoto ili media yenu ikue kwa speed
ReplyDeletepia wekeni online tv
ReplyDelete