WATU 18 wamenusurika kufa
baada ya basi dogo lenye namba T 565 DKV la Kampuni ya Magumba
Express walilokuwa wakisafaria kutoka Bariadi mkoani Simiyu kwenda
Nzega mkoani Tabora kuacha njia na kupindukia mtaroni wakati likijaribu
kulipita gari lenye namba T 933 EKQ aina ya Toyota Mark 11.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa
hospitali hiyo, Dkt Bwire Robert amekiri kupokea majeruhi hao (wanaume
15 na wanawake watatu) Jumatatu saa 3:00 asubuhi na amesema hali za wengi wao
zinaendelea kuimarika isipokuwa mmoja anayepelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando
mkoani Mwanza kwa ajili ya matibabu ya kibingwa zaidi.
No comments:
Post a Comment