NEWS

Thursday, 11 June 2020

RPC TarimeRorya: Uchunguzi kifo cha Mwalimu Rich unaendelea




Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi TarimeRorya, William Mkonda, amesema uchunguzi wa chanzo cha ajali ya moto iliyokatisha maisha ya Mwalimu wa Shule ya Msingi Azimio ya mjini Tarime, Richard Leonce, umeanza huku ukishirikisha taasisi mbalimbali za Serikali.

Tumeanza uchunguzi kujua chanzo kwa kushirikiana na wenzetu wa fire [Jeshi la Zima Moto na Uokozi] na Tanesco, RPC Mkonada ameimbia Mara Online News leo Juni 11, 2020.

Mwalimu Richard alifariki dunia jana Jumatano asubuhi nyumbai kwake baada ya kutokea ajali ya moto ambayo pia ilimjeruhi vibaya mke wake, Happiness Munisi na mtoto wao, Bright.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages