Wakulima wakiandaa kahawa kabla ya kuiuza |
BODI ya Kahawa Tanzania (TCB) imefungua msimu wa ununuzi wa
kahawa katika mkoa wa Mara huku ikitupilia mbali ombi la Wakulima wa Mara
Cooperative Union (WAMACU) Litd la
kepewa upendeleo wa kuwa mnunuzi pekee wa zao hilo kwa maelezo kuwa hali hiyo
inaweza kuwanyima wakulima raha.
“Tumefungua msimu na yeyote anayetoa bei nzuri kwa wakulima
ni ruksa. Sisi tunachotaka ni mkulima apate raha,” Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
TCB, Profesa Jamal Adam, ameimbia Mara Online News kwa njia ya simu jana Julai
1, 2020.
Profesa Adam amesema hadi sasa kampuni mbili zimeshapewa
leseni ya kuanza kununua kahawa katika wilaya ya Tarime mkoani Mara, akizitaja
kuwa ni Kijani Hai na CMS.
“Sisi tunachotaka ni mkulima apate raha iwe ni kutoka kwa
Kijani Hai, au CMS, au WAMACU,” amesisitiza Kaimu Mkurugenzi huyo wa TCB.
“WAMACU
akibaki mwenyewe mkulima hawezi kuwa na furaha katika mahali ambapo hakuna
ushindani.,” amesema Profesa Adam
No comments:
Post a Comment