NEWS

Thursday, 2 July 2020

TRA Mara yatangaza mfumo mpya wa ukusanyaji kodi



 Zake Wilbard Rwiza akizungumza katika semina hiyo
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanzisha mfumo mpya unaolenga kuboresha na kurahisisha ukusanyaji na ulipaji kodi za serikali.
Akizungumza katika semina kwa wafanyabiashara mbalimbali mjini Tarime leo Julai 2, 2020, Afisa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi wa TRA Mkoa wa Mara, Zake Wilbard Rwiza, amesema mfumo huo ujulikanao kama RGS, unatoa huduma isiyo na karaha kwa walipakodi.
Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia mafundisho katika semina hiyo

“Watumiaji wakubwa wa mfumo huu ni TRA, Benki Kuu, walipakodi na washikadau wengine,” amesema Rwiza na kuongeza “Unamwezesha mdau kulipa kodi kwa njia ya mtandao na hata simu ya mkononi.” 

Ametaja faida nyingine za mfumo huo kuwa ni pamoja na mtumiaji kurekebisha makosa kabla ya kutuma taarifa, lakini pia kuwezesha Wizara ya Fedha kujua makusanyo ya mapato ya serikali kwa wakati.

(Imeandikwa na Mara Online News, Tarime)


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages