NEWS

Tuesday 6 October 2020

Mafuriko ya Waitara Gorong'a

 
Wananchi wa kata ya Gorong'a wakimshangilia mgombea ubunge jimbo la Tarime vijijini kwa tiketi ya CCM  Mwita Waitara leo jioni 

Mamia ya wananchi wa kata ya Gorong'a leo Jumanne Oktoba 6,2020   wamejitokeza  kumsikiliza  mgombea ubunge wa jimbo la Tarime vijijini kwa tiketi ya CCM Mwita Waitara  ambapo Waitara pamoja na mambo mengine ameahidi kujenga vyoo katika minada mbalimbali   akipata ridhaa ya wananchi  kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Waitara akikagua moja ya kadi ya wanachama wa CHADEMA waliojiunga na CCM katika mkutano huo leo  

Mapema leo asubuhi  Waitara aliwasili  katika kitongoji cha Nyamichele, kijiji cha Nyakunguru na kusikiliza malalamiko ya wananchi wanaodai fidia  ya ardhi kutoka  mgodi wa North Mara na kuahidi  kusadia wananchi wa eneo hilo kupata malipo yao. 

 

Waitara akiwa Nyamichele leo mapema

 Baada ya hapo Waitara aliendelea na mikutano yake ya kampeni ambapo pia alifanya mkutano wa kampeni katika kijiji cha Karakatonga , kata Nyarokoba .  

                                               Sehemu ya wananchi wa Karakatonga wakimsikiliza Waitara leo  mchana

  Waitara anachuana na John Heche wa CHADEMA pamoja  na Charles Mwera wa ACT-Wazalendo 


Picha na Mara Online News)

  

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages