NEWS

Friday 9 October 2020

Waitara aahidi kuipandisha hadhi sekondari ya Inchugu

Mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini kupitia CCM, Mwita Waitara akijinadi katika mkutano wa kampeni kijijini Ketagasembe leo.

MGOMBEA ubunge jimbo la Tarime Vijijini kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara leo Oktoba 9, 2020 amefanya mkutano wa kampeni katika kijiji cha Ketagasembe, kata Gwitiryo na kuahidi kuwa akichaguliwa atahakikisha Shule ya Sekondari ya Inchgu inapewa hadhi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha tano na sita.

 “Kuanzia  mwakani mwezi wa tano Inchugu Sekondari itakuwa inaitwa Inchugu high school,” Waitara ambaye pia ni Naibu Waziri wa TAMISEMI amesema wakati akijibu ombi la mgombea udiwani kata Gwitiryo kwa tiketi ya CCM, Nashoni  Mchuma.

 

Pia Waitara ameahdi kuhakikisha kijiji cha Ketagasembe kinaunganishiwa umeme kabla ya mwezi huu wa Oktoba kuisha.

 

“Kata ya Gwitiryo pia itapata kituo cha afya chini ya Waitara na Mchuma,” ameongeza mgombea huyo.

Wananchi wakimshangilia mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara (hayupo pichani) katika mkutano wa kampeni kijijini Ketagasembe leo.

 

Waitara pia amesema Ketagasembe ni miongoni mwa vijiji vya kata ya Gwitiro ambavyo vitaunganisha na mtandao wa mradi wa maji unaotekelezwa katika mji mdogo wa Sirari.

 

Katika kinyang’anyiro hicho, Waitara anachuana Charles Mwera wa ACT - Wazalendo na John Heche wa Chadema.

 

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages