NEWS

Thursday 1 October 2020

Waitara afunika Nyamongo

Mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara akimwaga sera zake kwa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Nyamongo leo.


MGOMBEA ubunge jimbo la Tarime Vijijini kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara, leo Oktoba 1, 2020 ameuteka mji wa Nyamongo na vitongoji vyake kwa kupata mahudhurio makubwa ya wananchi katika mkutano wake wa kampeni.

 

Katika mkutano huo uliofurika mamia ya wakazi wa vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Waitara amewaomba kumchagua yeye na wagombea wengine wa CCM kwa mtindo wa mafiga matatu [rais, mbunge na madiwani].

Mamia ya wananchi wakimshangilia mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini kupitia CCM, Mwita Waitara katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Nyamongo leo.

 

Pamoja na mambo mengine, Waitara ameahidi kuupandisha hadhi mji wa Nyamongo kuwa mamlaka ya mji mdogo baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

 

Waitara pia ameahidi kwamba akichaguliwa kuwa mbunge wa Tarime Vijijini atatumia nafasi hiyo kuishawishi na kuiomba serikali kuweka lami katika barabara za mitaa ya mji wa Nyamongo, miongoni mwa huduma nyingine za kijamii.

 

#MaraOnlineNews-Updates

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages