NEWS

Wednesday 21 October 2020

Waitara apata mapokezi ya kishindo kijijini kwao Kangariani

Kikundi cha ngoma ya asili kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini kwa tiketi ya CCM, Mwita Waitara (hayupo pichani) kijijini kwao Kangariani jana.

 

MGOMBEA ubunge jimbo la Tarime Vijijini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwita Waitara jana amefanya mkutano wa kampeni kijijini kwao Kangariani ambapo alipata mapokezi makubwa wananchi yaliyotawaliwa na shangwe za aina yake.

Wananchi wa kijiji cha Kangariani wakimsikiliza Mwita Waitara akimwaga sera katika mkutano wake huo wa kampeni jana.

 

Katika mkutano huo uliotumbuizwa na ngoma za asili, mamia ya wakazi wa kijiji hicho kilichopo kata ya Itiryo wamemhakikishia Waitara kuwa wameshafanya maamuzi ya kumchagua kuwa mbunge wao, lakini pia kumchagua Dkt John Magufuli kuwa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania na Shadrack Marwa kuwa diwani wa kata ya Itiryo.


Wanawake wakicheza ngoma ya asili wakati wa mapokezi ya mgombea ubunge Jimbo la Tarime Vijijini kupitia CCM, Mwita Waitara kijijini Kangariani jana.


Waitara amehakikishiwa ahadi kama hiyo na wakazi wa kata ya Muriba alikokwenda kuhutubia mkutano mkubwa wa kihistoria baada ya kutoka Kangariani, Itiryo.

 

Mvua iliyonyesha haikuwazuia wananchi kuvutika kumsikiliza na kumshangilia Waitara katika mkutano wake wa kampeni katani Muriba na ilitafsiriwa na wengi kuwa ni ishara ya baraka ya ushindi wa mgombea ubunge huo.

Mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini kupitia CCM, Mwita Waitara akihutubia mkutano wa kampeni kijijini kwao Kangariani jana.

 

Wakati huo huo, leo Oktoba 21, 2020 Waitara amehutubia mikutano mikubwa ya kampeni katika kijiji cha Nyabichune (katani Regicheri) na Nyabisaga (Pemba) ambako amepata mapokezi makubwa ya mamia ya wananchi walioahidi kumpa kura za kishinda na wagombea wa CCM kwa nafasi za urais na udiwani. 

Mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini kupitia CCM, Mwita Waitara (wa tatu kushoto) akipokewa katika kijiji cha Nyabichune katani Regicheri leo.
 

Mwita Waitara akipokewa kwa tumbuizo la ngoma ya asili katika kijiji cha Nyabisaga katani Pemba alikohutubia mkutano mkubwa wa wananchi leo. (Picha zote na Peter Hezron)

Mgombea huyo ameendelea kutaja vipaumbele vyake endapo atachaguliwa kuwa ni pamoja na kuboresha sekta za elimu, afya, barabara, maji, umeme na mikopo kwa vijana na wanawake katika jimbo la Tarime Vijijini.

 

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages