NEWS

Tuesday 5 January 2021

Aweso, Waitara wateta jambo

 

Karibu Tarime Mheshimiwa Waziri. Ndivyo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita  Waitara (kushoto) ambaye pia ni Mbunge wa Tarime Vijijini anavyoonekana kumwambia Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ambaye amefanya ziara ya kukagua miradi ya maji wilayani Tarime, leo Januari 5, 2021. Waziri Aweso yupo mkoani Mara kukagua miradi mbalimbali ya maji hadi Januari 7, 2021.


Naibu Waziri Waitara (kushoto) akimweleza Waziri Aweso (katikati) kero  ya ukosefu wa maji safi wilayani Tarime katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, leo Januari 5, 2021. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon. (Picha zote na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages