NEWS

Monday 4 January 2021

Ziara ya Mbunge Waitara Tarime Vijijini katika picha, kutafuta ufumbuzi mgogoro wa mpaka wa hifadhi na wanavijiji


Mbunge wa Tarime Vijiji, Mwita Waitara ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara akizungumza na wakazi wa kata ya Nyanugu katika kutano wa hadhara uliofanyika kijijini Kegonga jana Januari 4, 2021, ambapo ameahidi kuwasilisha malalamiko yao kwa mamlaka husika kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa mgogoro wa kugombea mpaka kati yao na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara akihutubia mkutano huo wa kujadili namna ya kupata ufumbuzi wa mgogoro wa kugombea mpaka kati ya wanavijiji na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.


Diwani wa Kata ya Nyanungu katika Jimbo la Tarime Vijijini, Richard Tiboche akizungumza katika mkutano huo jana Januari 4, 2021. Waliokaa kulia ni Mbunge wa jimbo hilo, Mwita Waitara na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kegonga, Warioba Mogoyo.

Mwanakijiji akizungumza katika mkutano huo kijijini Kegonga jana Januari 4, 2021.

Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime Hamis Kura, akizungumza na wananchi katika mkutano huo jana Januari 4, 2021.

       Mwanakijiji mwingine akichangia mada katika mkutano huo jana Januari 4, 2021.


#Mara Online News-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages