NEWS

Monday 4 January 2021

Waziri Aweso kukagua miradi ya maji Mara, iliyopo vijijini kumulikwa zaidi

Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso, leo Januari 5, 2021 anaanza ziara ya siku tatu ya kukagua miradi ya maji mkoani Mara, huku iliyopo vijijini ikiangaziwa zaidi.

 

Katika ziara hiyo, Waziri Aweso atakagua miradi tisa ya maji katika wilaya za Tarime, Rorya, Musoma na Bunda kabla ya kikao kitakachofanyika mjini Musoma Januari 7, 2021 kwa ajili ya kupewa taarifa ya jumla ya hali za utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi mkoani Mara na baadaye kuhitimisha kwa kikao cha majumuisho mjini Bunda.

Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso
 

Ratiba inaonesha kuwa miradi mingi itakayokaguliwa na Waziri Aweso ipo maeneo ya vijijini. Miradi hiyo na wilaya ilipo ikiwa kwenye mabano ni Gamasara, Magoma, Nyantira na Nyarwana (Tarime), Komuge, Ingri Juu na Shirati (Rorya), Bulinga – Bujaga (Musoma) na mradi wa chujio la maji Nyabehu (Bunda).

#Mara Online News-Updates

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages