NEWS

Wednesday 20 October 2021

Mbunge Ghati abeba wabunge wa Mara madhimisho wiki UWT kitaifa


MJUMBE wa Baraza Kuu la jumuiya ya CCM ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Rhobi Samwelly amewashukuru wabunge wa mkoani Mara waliotoa michango ya fedha kuwezesha viongozi wa jumuiya hiyo kuhudhuria maadhimishoya kilele cha Wiki ya UWT Kitaifa.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Rhobi jana,maadhimisho hayo yatafanyika  Oktoba 23, 2021 kwenye viwanja vya Ujamaa, Rufiji Ikwiriri mkoani Pwani.
Ghati akishiriki moja ya kikao cha Bunge jijini Dodoma    
 
Amesema Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Zephania Chomete amechangia shilingi milioni 2.5, Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, (laki 3), Mbunge wa Rorya, Jafari Chege (laki 2 na elfu 10), Mbunge wa Butiama, Jumanne Sagini (laki 2), huku yeye mwenyewe [Rhobi] akichangia shilingi 590,000.

Rhobi (pichani juu) amesema shilingi milioni 3.8 zitatumika kugharimia usafiri wa wajumbe kutokwa Musoma kwenda Rufiji na kurudi Musoma.
 
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan.

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ya  kilele cha Wiki ya UWT Kitaifa inasema "Tushiriki Kumkomboa Mwanamke Kiuchumi, Kifikra na Kisiasa".

#MaraOnlineNews-Updates

1 comment:

  1. Hakika penye Nia Pana njia!
    Mungu Mwema aendelee kuwatunza wote walioshiriki katika kuiwezesha safari ya UWT-Mara.
    Tunawaombea Kila la Kheri katika safari kina Mama wawakilishi toka Mara.

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages