NEWS

Monday, 16 December 2024

TAMISEMI yatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2025



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa alitangaza kuwa jumla ya wanafunzi 974,332 waliohitimu Elimu ya msingi mwaka 2024 tayari wamepangiwa Shule za sekondari ambapo watajiunga  Januari 2025.

Waziri Mchengerwa alitangaza matokeo hayo mbele ya vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam Disemba 16, 2024.

Wanafunzi waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) mwaka 2024,ambao walipata alama kati ya 121 hadi 300,wamepangiwa shule za sekondari za serikali.Wanafunzi wenye alama za juu wameweza kuchaguliwa katika shule za vipaji au shule za bweni.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages