NEWS

Friday, 18 April 2025

Seleman Mwalimu kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Kombe la Dunia la Vilabu



Seleman Mwalimu

Mchezaji kinda raia wa Tanzania anayeitumikia klabu ya Wydad Athletic Club "Wydad Casablanca" ya nchini Morocco, Seleman Mwalimu, anakaribia kuweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Kombe la Dunia la Vilabu litakaloanza Juni 14 hadi Julai 13, mwaka huu wa 2025 nchini Marekani.

Seleman Mwalimu anayecheza soka la kulipwa nchini Morocco katika klabu ya Wydad Casablanca atapata fursa ya kuweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza michuano hiyo mikubwa ngazi ya vilabu, kutokana na ushiriki wa klabu yake hiyo katika mashindano hayo.

Nyota huyo ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" alijiunga na miamba hiyo ya soka la Morocco na Afrika kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea Fountain Gate FC inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Timu 32 kutoka mabara yote duniani zinatarajiwa kuchuana vikali kusaka ubingwa wa kwanza wa mashindano hayo wenye muundo mpya wa uendeshaji tofauti na ule wa awali ulioshirikisha timu saba pekee.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages