NEWS

Wednesday 13 October 2021

Mbunge Ghati avipa heko vyombo vya Mara Online kwa habari za kuhamasisha maendeleo




MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Zephania Chomete (pichani juu kulia), amevipongeza vyombo vya habari; Blogu ya Mara Online News na Gazeti la Sauti ya Mara, kwa kazi nzuri ya kuilisha jamii habari zinazohamasisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mbunge Ghati ametoa pongezi hizo wakati alipozuru ofisi za vyombo hivyo vya habari mjini Tarime na kufanya mazungumzo maalumu na wahariri wake, leo Oktoba 13, 2021.


Mhariri Mkuu, Christopher Gamaina (kushoto) akimuonesha Mbunge Ghati nakala ya toleo la wiki hii la Gazeti la Sauti ya Mara, huku Mhariri Mtendaji, Jacob Mugini (mwenye tai) na diwani aliyefuatana na mbunge huyo kutoka Musoma wakifurahia tukio hilo.

Amesema vyombo hivyo vimekuwa mstari wa mbele katika kuibua na kuandika habari zinazohamasisha wadau kujitokeza kuchangamkia fursa lukuki za uwekezaji katika sekta za elimu, madini, utalii, uhifadhi, kilimo, uvuvi, ufugaji, viwanda na michezo mkoani Mara.

Pia habari za kuhamasisha usawa wa kijinsia, kukemea mila na desturi kandamizi kwa watoto wa kike na kuonesha maendeleo yanayowezeshwa na wanawake viongozi katika jamii.


Mbunge Ghati (wa nne kutoka kulia) na madiwani aliofuatana nao kutoka Musoma (wa kwanza na wa pili kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mara Online. Wa tatu kutoka kulia ni Mhariri Mtendaji, Jacob Mugini.

Mbunge huyo amewatia moyo wahariri na waandishi wa habari wa vyombo hivyo kuendelea kuandika habari za kweli zinazochochea maendeleo ya mkoa wa Mara na Taifa kwa jumla.

(Habari na picha: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages