NEWS

Friday 19 November 2021

Serikali yapeleka milioni 250/- kuchangia ujenzi wa kituo cha afya kisiwa cha Rukuba Musoma VijijiniMbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo

SERIKALI ya Awamu ya Sita imetoa Sh milioni 250 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa kituo cha afya katika kisiwa cha Rukuba kilichopo kata ya Etaro, Musoma Vijijini.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini kwa vyombo vya habari, hivi karibuni.

Kulingana na taarifa hiyo, wananchi wa eneo hilo walishaanza kupanua zahanati iliyopo kwa kujenga wodi ya mama na mtoto, hivyo wanachokifanya sasa ni kuendelea na ujenzi wa kuipanua iwe kituo cha afya.

“Asante sana Serikali yetu, asante sana Rais wetu Samia Suluhu Hassan,” sehemu ya taarifa hiyo imesema.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages