NEWS

Tuesday 26 April 2022

Mbunge Kembaki amwaga misaada lukuki Gereza la TarimeMBUNGE wa Tarime Mjini, Michael Kembaki, leo Aprili 26, 2022 amezuru katika Gereza la Tarime mkoani Mara na kutoa msaada wa bidhaa mbalimbali kwa ajili ya wafungwa na mahabusu.

Msaada huo ambao ameukabidhi kwa Mkuu wa Gereza hilo, Sebastian Dioniz, ni pamoja na TV ya inchi 50 yenye thamani ya shilingi milioni 1.3 na kuilipia kifurushi cha mwaka mzima, katoni 40 za soda na katoni 40 za sabuni na fedha taslimu shilingi 500,000 kwa ajili ya kununua chakula cha wafungwa na mahabusu.

Mbunge Kembaki (mwenye shati la drafti akikabidhi misaada hiyo kwa Mkuu wa Gereza, Dioniz.

Aidha, Mbunge Kembaki ameahidi kutoa msaada wa saruji mifuko 50 na matofali kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati ya gereza hilo.

Ametumia nafasi hiyo pia kusikiliza wafungwa na mahabusu ambao wamemueleza kero zinazowakabili, ikiwemo uchakavu wa miundombinu ya vyoo, ambapo ameahidi kuzifikisha kwa mamlaka husika kwa hatua za ufumbuzi.

Hata hivyo, Mbunge Kembaki ameupongeza uongozi na watumishi wa gereza hilo kwa kujenga uhusiano na wafungwa na mahabusu. Nkuu wa Gereza, Dioniz amemshukuru mbunge huyo kwa ziara na msaada huo.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages