NEWS

Thursday, 28 April 2022

Mbunge Chege aibana Serikali kupeleka maji mbadala kwa wanavijiji wa jimboni Rorya walioathiriwa na uchafuzi wa Mto Mara



MBUNGE wa Rorya mkoani Mara, Jafari Chege (pichani aliyesimama), amehoji Bungeni - akitaka kujua Serikali imefikia hatua gani ya utekelezaji wa ahadi ya kupeleka maji mbadala kwa wanavijiji wa jimbo hilo walioathiriwa na uchafuzi wa Mto Mara.

“Vijiji vilivyoathirika na machafuko ya mto Mara ni pamoja na kijiji cha Kwibuse, Marasibora na Kyamwame, na Serikali iliahidi kupeleka maji mbadala kwenye vijiji hivi ambavyo havitumii maji haya kwa sasa.

“Nataka nijue Serikali imefikia wapi kwenye mpango huu kuhakikisha wale wananchi wanapata maji safi na salama?” Mbunge Chege amehoji Bungeni jijini Dodoma leo.

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi alipotakiwa na Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson kujibu swali hilo, amesema kwa kifupi bila ufafanuzi “Nimepokea tutawasiliana na Mheshimiwa Mbunge.”

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages