NEWS

Thursday 16 March 2023

Gachuma ammiminia Rais Samia sifa akizindua chombo cha habari cha Lake Zone Watch jijini Mwanza


Mjumbe wa NEC, Christopher Mwita Gachuma (wa pili kushoto) na CEO wa Lake Zone Watch (kushoto) wakionesha leseni ya usajili wa chombo hicho cha habari.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
-------------------------------------------

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Christopher Mwita Gachuma amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa anazofanya kuiletea nchi maendeleo mikubwa ya kisekta.

Mhe. Gachuma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba nchini, ameyasema hayo katika hotuba yake ya uzinduzi wa chomba cha habari cha Lake Zone Watch jijini Mwanza leo.

“Ninamshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Rais Samia kwa juhudi zake za kuendeleza na kukamilisha miradi mikubwa ya maendeleo kama ile ya umeme, SGR (reli ya kisasa) na daraja la kwenda Sengerema [Kigongo - Busisi mkoani Mwanza].

Kwa upande mwingine Gachuma ameupongeza uongozi wa Lake Zone Watch kwa ubunifu wa kuanzisha chombo hicho cha habari na ofisi zake jijini Mwanza, huku akitumia fursa hiyo pia kuhimiza uandishi wa habari za kweli na zenye maslahi kwa taifa.

“Waandishi wa habari ni watu muhimu sana, lakini ukipotosha habari unaweza kuharibu vitu vingi, hivyo lazima muwe makini, watu wanataka habri za maana, za kweli na za kuelimisha,” Gachuma amesisitiza.

Naye Mjumbe wa NEC ya CCM, Joyce Ryoba Mang’o ambaye alianza kwa kuzindua ofisi za Gazeti la Sauti ya Mara na Lake Zone Watch jijini Mwanza, amempongeza Afisa Mtendji Mkuu (CEO) na Mhariri Mtendaji (ME) wa vyombo hivyo vya habari, Jacob Mugini akisema ni mfano mzuri wa kuigwa katika masula ya ubunifu na kujiajiri.

Mjumbe wa NEC, Joyce Mang'o (katikati) akifurahia uzinduzi wa ofisi za Sauti ya Mara na Lake Zone Watch jijini Mwanza leo.

Awali, CEO Mugini akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema Lake Zone Watch kitakuwa chombo cha habari cha kwanza kitakachokuwa kikichapisha habari na makala kwa lugha ya Kiingereza mtandaoni (internet) na hivyo kusaidia kuiunganisha mikoa ya Kanda ya Ziwa na wadau muhimu wa maendeleo wakiwemo wawekezaji, watalii na mashirika yasio ya kiserikali ya kitaifa na kimataifa yanayotekeleza, au kufadhili miradi ya kijamii katika Kanda ya Ziwa.

“Ili kufikia lengo hili chombo hiki kitajikita katika kutoa taarifa za kweli kwa kuzingatia weledi wa hali ya juu huku tukizingatia maslahi ya taifa letu kwanza na mwisho wa siku tuwe sehemu ya maendeleo ya Kanda Ziwa.

“Habari na makala zetu zitaangazia zaidi sekta za madini (minerals), uhifadhi (conservation), utalii (tourism), maji, ujenzi, kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo pamba na kahawa. Pia tutazipa kipaumbele habari za elimu kwa watoto wa kike na kusaidia kutoa elimu juu ya mila zinazokatisha ndoto zao za kielimu.

“Kipaumbele chetu kingine kitakuwa kuonesha miradi maendeleo ya miradi mikubwa ambayo inatekelezwa na Serikali ya Awmu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa na uboreshaji wa miundombinu ambayo itasaidia kuharakisha maendeleo ya kiuchumi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

“Pia tutakuwa tunachapa makala za habari za mafanikio, yaani success stories ya miradi ambayo inatekelezwa na Serikali katika sekta za elimu, afya na maji bila kusahau kuonesha changamoto zilizopo kwa lengo la kutaka mamlaka husika zione na kuchukua hatua (stories triggering solutions),” amesema Mugini.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages